Wednesday, 25 January 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuendesha gari la Mwendo Kasi katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) Gerezani, Kariakoo jijini Dar es Salaam, Januari 25, 2017. Rais amezindua mradi huo ambao ni awamu ya kwanza, na kuagiza waendesha mradi kujenga vituo  viwili vikubwa eneo la Kimara mwisho  vitakavyotumika kama maegesho ya daladala na magari madogo ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji. (PICHA ZOTE NA IKULU/MAELEZO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua moja ya basi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakati Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka kadi ya Kieletroniki katika Mashine ya UDART ilikuweza kupita kama ishara ya Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene akimuelekeza jambo katika mashine hizo.

 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop, akitoa hotuba yake.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop akimtunza msani Mrisho Mpoto wakati alipokuwa akitumbuiza katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka BRT-Kariakoo huku Rais Dkt. Magufuli akifurahia.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda alitoa hotuba ya ukaribisho

Reactions:

0 comments:

Post a Comment