Monday, 16 January 2017

 Profesa Palamagamba Kabudi
NA K-VIS BLOG
RAIS wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzanoa, Dkt. John Pombe Magufuli, amewateua, Profesa Palamagamba Kabudi na Alhaj Abdallah Majura Bulembo, kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Bw.Gerson Msigwa na kusambazwa kwenye vyombo vya habari leo Januari 16, 2017, Rais pia amemteua Bw.Benedicto Martin Mashiba, kuwa balozi.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa, wakati wabunge hao wataapishwa kwa mujibu wa taratibu za kibunge, Bw. Mashiba atapangiwa kituo chake cha kazi baadaye.

 Alhaj Abdallah Bulembo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment