Thursday, 19 January 2017

 RAIS John Pombe Magufuli, leo Januari 19, 2017 amepokea taarifa ya maendeleo ya usuluhishi wa mzozo wa kisiasa nchini Burundi, toka kwa msuluhishi, Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Rais Mkapa, alisema mazungumzo yao yalilenga kumpa taarifa Rais Magufuli kama Mwneyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya mkutano wa usuluhishi uliofanyika majuzi mjini Arusha, baina ya wawakilishi wa serikali ya Burundi na makundi yanayovutana. "Mkutano wa wakuu wa Afrika Mashariki nadhami wanakutana mwezi ujao kwa hivyo nilifika kumpa update(maendeleo) ya mazungumzo hayo." Alinukuliwa Mkapa akiwaambia waandishi wa habari. (PICHA NA IKULU)
Rais John Pombe Magufuli, akiongozana na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 19, 2017.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment