Wednesday, 11 January 2017RAIS john Pombe Magufuli, amewaambia Watanzania kuwa, ana habari kuwa wapo wafanyabiashara, wanaoingiza vyakula nchini, wanakula njama na wanasiasa na baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa lipo tishio la njaa nchini.
Rais ameyasema hay oleo Januari 11, 2017 wakati akihutubia wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu muda mfupi baada ya kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilomita 71.8.
“Rais ndiye anayejua kama njaa ipo au haipo, kuna mfanyabiashara anamatani ya mahindi bandarini, anashawishi baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa kupiga kelele kuwa Tanzania kuna njaa, ili vyakula alivyoingiza visamehewe kodi, namwambia hivi kodi sisamehi na atalipa.” Alisema.
Rais pia amemsifia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka, kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, kwa kuanzisha viwanda kiwilaya.
Rais pia amekataa bajeti ya shilingi bilioni 46 ya ujenzi wa jengo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu ambalo pia ameweka jiwe la msingi.
“Mimi sitoi hizo pesa, na badala yake nitatoa shilingi bilioni 10 kujenga jingo hilo na nitakuja mimi mwenyewe kulifungua, nadhani Waziri wa Ujenzi, na Mkuu wa Mkoa mmenielewa.” Alisema.
Rais amewataka watanzania kufanya kazi, na kurejea kauli yake kuwa serikali anayoiongoza haitagawa chakula cha bure. "Ndugu zangu naomba tuelewane katika zama hizi za kusema ukweli, tulizoea maneno matamu, na sasa tuzoee maneno machungu, lakini kwa manufaa ya Watanzania" Alisema.


Rais Dkt.John Pombe MAGUFULI, na viongzo wa serikali na Ccm, akizindua barabara ya kilomita 71.8 ya kiwango cha lami kutoka Bariadi hadi Lamadi mkoani Simiyu Leo Januari 11, 2017.(PICHA NA IKULU).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment