Saturday, 14 January 2017NA DAUDI MANONGI-MAELEZO.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo  ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff  ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji  marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizoifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu kwani ni urithi wa kila mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huu wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.


RaisMsataafuwa Benjamin Mkapa, akihutubia baada ya matembezi hayo ya kilomita 5 ya "

Walk for Elephant Dar es Salaam 2017" yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Januari 14, 2017.


Baloziwa China nchini Dkt. Lu Youqing, akizungumza


Katibu Mkuuwa Asasi ya Tanzania – China Promotion Association,(TCFPA), Joseph Kahama, akizungumzia dhima ya kuandaa matembezi hayo.

 Balozi wa China Dkt. Lu Youqing, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kionondoni, Ally Hapi
 Pasha pasha baada ya matembezi
 Matembezi yakiendelea na Msanii Mrisho Mpoto nae alikuwepo
Msanii Mrisho Mpoto, na kundi lake la Mjomba Band, akitoa burudani. (PICHA ZOTE NA
FRANK SHIJA – MAELEZO).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment