Monday, 16 January 2017


NA K-VIS BLOG
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la kupandisha bei za vyakula.
Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo(Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.
“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatuhali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.
Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.
“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.
Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma  baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka  uwanja wa ndege  wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo  kati ya viwanja viwili hivi. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka   uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere,  Dar es salaam kwenda Dodoma Januari  16, 2017.  Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)  kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo.  Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,   Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania   (ATCL)   Januari 16, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  ​  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania   (ATCL)    kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016.  Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ngege ya Tanzania (ATCL) baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni  uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza katika uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la  Tanzania (ATCL) kati ya uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma Januari 16, 2017Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni  uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017
Reactions:

0 comments:

Post a Comment