Monday, 16 January 2017NA K-VIS BLOG
ALIYEKUWA Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Edward Lowassa, amekamatwa na polisi mkoani Geita akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Nkome mkoani hum oleo Januari 16, 2017.
Taarifa kutoka Geita zinasema, pamoja na Bw. Lowassa, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Geita, Bi. Upendo Furaha Peneza, naye pia amekamatwa. Bi Peneza alikuwa kwenye msafara wa Bw. Lowassa.
Taarifa zaidi zinasema, Bw. Lowassa alikumbana na “mkono wa dola” baada ya kusimamishwa na wananchi waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabara na hapo msafara wake ulisimama na kuanza kuwasalimia, kitendo ambacho wapasha ahabari wanasema kiliwafanya polisi kumtia mbaroni na kuamuru msafara wake uelekee kituo cha polisi.
“Msafara wa Bw. Lowassa ulikuwa ukitokea moani Kagera na ulipofika stendi ya zamani Geita wananchi wakamsimamisha, aliposhuka kwenye gari kuwasalimu wanageita, polisi wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Geita.” Mmoja wa mashuhuda alisema.

Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema, Bw. Lowassa ameachiwa huru baada ya kuhojiwa na polisi na msafara wake sasa umeelekea mkoani Mwanza.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment