Thursday, 5 January 2017


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria Uzinduzi rasmi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja Januari 5, 2017. Uzinduzi huo ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto). (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)

NA K-VIS BLOG

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekifungua kiwanda kikubwa na cha kisasa cha Maziwa  cha “Azam Dairy” na kueleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyokusudia kuimarisha na kuendeleza viwanda ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Sekta binafsi.


Dk. Shein aliyasema hayo, katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya kukizindua rasmi kiwanda hicho kinachomilikiwa na  Bakhressa Group of Campanies” inayoongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Said Salim Bakhressa, kilichopo Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya matukufu ya Zanzibar.
Taarifa kamili ya uzinduzi huo inapatikana hapo chini


Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Maziwa cha (Azam Dairy Products Ltd.) wakiendelea na shuhuli zao za kuhakikisha maziwa yanapangwa vizuri katika maboksi katika hatua za mwisho kuelekea  sokoni

Dkt. Shein akipokelewa na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakhresa alipowasili kuzindua rasmi kiwanda hicho

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha Maziwa cha AZAM Dairy Products Ltd,  Adilson Fagundes, (kushoto)
Mwakilishi wa Kampuni ya Azam Diary Bw.Salim Aziz akitoa maelezo kuhusu mradi wa uzalishaji wa maziwa katika uzinduzi wa Kiwanda cha Maziwa  cha (Azam Dairy Products Ltd.)

Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.)
Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.)

Baadhi ya wananchi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment