Thursday, 12 January 2017


NA FRANK SHIJA – MAELEZO
ZANZIBAR imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali za kimaendeleo na utoaji wa huduma bora za kijamii.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, (pichani juu), wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi leo katika uwanja wa Amani, Unguja, Zanzibar.
Dkt. Sein amesema kuwa siku ya Mapinduzi ni muhimu sana katika historia ya Zanzibar kwani ndiyo siku ambayo Wazanzibar walipokuwa huru katika nchi yao na kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maaendeleo.
“Tukiwa tunasherehekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vyema tukajivunia maendeleo yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.”Alisema Dkt. Shein.
Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi Matukufu yatokee tarehe 12 Januari 1961, Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka shule 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843 mwaka 2016.
Ongezeko hilo limeenda sambamba na ongezeko la udahili wa wananfunzi ambapo umeongezeka kutoka wanafunzi 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.
Katika sekta ya afya kumekuwa na mafanikio ya kuongezeka kwa vituo vya afya kwa asilimia 13.4 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 134 hadi kufikia sasa jumla ya Vituo 152 vimepatikana.
Mafanikio mengine ni pamoja na upatikanaji wa ajira 2658 zilizotokana na miradi mbalimbali iliyozindulia katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya Mapinduzi, kukua kwa Sekta ya Utalii kwa ongezeko la watalii kwa asilimia 13 huku ikichangia pato la taifa kwa asilimia 27.
Huduma za kijamii zimezidi kuboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama umeendelea kutatuliwa ambapo miradi ya maji imeekuwa ikitekelezwa ikiwemo kuchimba visima vipya 9 na kuvifanyia ukarabati visima vya zamani.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa Mapinduzi haya yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka Wazanzibar kuwa huru katika kutekeleza shughuli zao za kujiletea maendeleo.
Zanzibar imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huku ikiwa imepiga hatua kubwa za kimaendeleo ambapo katika shamra shamra za maadhimisho haya jumla ya miradi 32 ya maendeleo imezinduliwa huku mingine 16 ikiwekwa jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji wake, hayo yote ni matunda yatokanayo na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo baadaye yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baadhi ya waandamanaji wakishangilia  wakati walipopita mbele ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed  Shein katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Zanzibar Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume akiteta na  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka  53 ya Mapinduzi  ya Zanzibar  zilizofanyika kwenye uwanja wa Aman Zanzibar Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sif Idd wakifuatilia kwa makini gwaride  la Maaddhisho ya miaka 53  ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mmoja wa wananchi wa Zanzibar akimsikiliza kwa makaini Rais wake, Dkt. Ali Mohammed Shein  wakati alipohutuba katika Maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwenye uwanja wa Aman Januari 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 


Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi cha Zanzibar akipita   kwa ukakamavu mbele ya  mgeni rasmi Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein  katika gwaride la kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)


Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha  jinsi matofari yanavyoweza kuvunjwa juu ya kichwa katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa  amelala  juu ya misumari  huku wenzake wakipita juu yake ikiwa ni moja ya maonyesho ya ukakamavu yaliyoonyeshwa na Makomandoo hao katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12. 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika Gari Maalum huku akiongozwa na Pikipiki za Polisi, akiwangia mkono wananchi waliohudhuria  katika Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe zilizofanyika leo Januari 12, 2017 kwenye uwanja wa Amaan Mjini Unguja. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Lt.Co.Khamis Mohamed Adam  wakati akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama
Baadhi ya Watendaji kutoka Idara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi wakiwa katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanziba,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja
Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe,Dkt.Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (katikati) alipowasili katika Uwanja wa Amaan
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Willium Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa (katikati)  walipowasili katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Kassim Majaliwa  Majaliwa

Gwaride la Farasi likimsindikiza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein alipoingia katika akiwa Uwanja wa Amaan Mjini Unguja
Reactions:

0 comments:

Post a Comment