Sunday, 29 January 2017


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma  kuja jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.
Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.
“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.
Habari mpya zilizotufikia kutoka kwa msemaji wa TRL, Midladjy, zinasema treni hiyo imeanguka majira ya saa 9:40 alasiri. "Treni yetu ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar kutoka Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali . Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu  yameacha njia..Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa.amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Hizi ni taarifa za awali..baada ya Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya Wahanga itakamilika! Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa Makame Mbarawa. .Mkuu wa TRL  Ndugu Kagosa Kamanda Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi Chillery wako njia kuelekea katika eneo la ajali! . Sehemu ya treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi  iko njiani kuja Dar es Salaam inatarajiwa kufika saa 2 usiku huyu., amesema Bwana Maez.
 Abiria na wasamaria wakiokoa abiria kutoka treni ya mwendo haraka ya Delux iliyokuwa ikitoka Kigoma kuja jijini Dar ES Salaam, baada ya kuanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.Reactions:

0 comments:

Post a Comment