Saturday, 14 January 2017


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabishi Kombe la Mapinduzi mwaka 2017 nahodha wa timu ya Azam Fc, John Bocco usiku wa kuamkia Januari 14, 2017, baada ya timu hiyo kuifunga Simba bao 1-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Amaan mjini Unguja, Zanzibar.(PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)NA K-VIS BLOG
TIMU ya mpira wa soka ya Azam FC, yenye maskani yake Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam, imetwaa kombe la Mapinduzi 2017, baada ya kuifunga Simba ya Dar es Salaam, bao 1-0 kwenye pambano la kupendeza la fainali lililopigwa uwanja wa Aman mjinu Unguja, Zamnzibar, usiku wa kuamkia leo Januari 14, 2017.
Bao lililoizamisha Simba, lilifungwa na beki wa Azam, kwenye daika ya 12 ya mchezo kwa shuti kali alilofumua nje ya sanduku la 18.
Rais wa Zamzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mainduzi, Dkt. Ali Mohammed Sjein ambaye alikuwa ,geni rasmk, ndiye aliyekabidhi kombe hilo kwa naohodha wa Azam, John Raphael Boko, na kitita cha shilingi Milioni 10, sambamba na medali za dhahabu kwa kila mchezaji na afisa wa timu hiyo.


 Dkt. Shein katika picha ya pamoja na wachezaji wa Aza Fc.
  Dkt. Shein katika picha ya pamoja na wachezaji wa Simba Sc.
 Mchezaji wa Azam Fc, Yahya Mohammed, (kushoto), akimenyana na kiungo wa Simba James Kotei

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwasalimia   wachezaji  wa Timu ya Simba   kabla mpambano wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Azam  katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja, Januari 14, 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwasalimia   wachezaji  wa Timu ya Azam   kabla mpambano wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Simba  katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Waamuzi wa mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi-2017, kati ya  Simba Sc na Azam Fc.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwavalisha nishani wachezaji wa timu ya Simba 
Reactions:

0 comments:

Post a Comment