Tuesday, 6 December 2016

 Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu na Meneja wa NMB, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), baada ya kufunga mkutao mkuu wa mwaka wa Mtandao huo jijini Dar es Salaam, Desemba 6, 2016


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye, amesema, Bloga, (Bloggers), ni kundi ambalo linachukua ushawishi mkubwa katika kuhabarisha umma katika wakati huu ambao teknolojia ya habari na mawasiliano imekuwa sana.

Waziri aliyasema hay oleo Desemba 6, 2016 wakati akifunga mkutano mkuu maalum wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), kwenye ukumbi wa mikutano wa jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
“Naona mmekuwa na eneo lenu linapata nguvu kubwa kwa sababu ya mabadiliko ya kasi sana ya sayansi na teknolojia Duniani, takwimu zinaonyesha leo hii watumiaji wa Internet Tanzania wamefika karibu milioni 20 na zaidi na karibu asilimia 80 ya kila mtu mwenye simu Tanzania anatumia internet utaona namna gani mmlivyo na nguvu ya kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja na kwa muitikio mkubwa.” Alisema.
Waziri Nape pia alisema, karibu social media zote, kama vile Facebook, Instagram, Tweeter zimekuwa connected na Blogs.
“Tunathamini mchango wenu mkubwa katika kuhakikisha sekta ya habari Tanzania inakuwa, na kama ulivyosema mwenyekiti, nyinyi mko Zanzibar na Bara lakini mmekwenda mpaka nje, hili ni jambo zuri na mnafanya kazi nzuri sana.” Alisema
Waziri alisema, katika watu waliochangia kuirudisha CCM madarakani, ni Bloggers, “Kuna mtu nilikutana naye pale Serena hotel, “Binafsi mimi leo nitawaambia siri moja, kabla ya kuwa waziri nilikuwa katibu mwenezi wa CCM, katika watu walioirudisha CCM madarakani ni Bloggers, kuna mtu mmoja nilikutana naye pale Serena wakati tunahangaika hivi, CCM wakati huo inatupiwa mawe kila kona kuandikika haiandikiki, akasema wewe Nape utahangaika bure, wewe si ndio katibu mwenezi, hawa jamaa wote huko utahangaika nao, wewe tafuta bloggers wachache, kaa nao wawaelewe halafu waanze kuandika habari zenu utaona mambo yanabadilika, kwakweli hali ikaanza kubadilika, taratibu taratibu mwishowe ikabadilika baadaye Magufuli akapatikana, kwa hivyo kiukweli, kiukweli, waliotusaidia sana kubadilisha image iliyokuwepo, kutoka ubaya kwenda image ambayo watu wakaendelea kuiamini CCM ni Bloggers.” Alifafanua.
Waziri Nape alisema anathamini sana mchango wa Bloggers na kusisitiza kuwa Bloggers watusaidie ku-shape direction ya wapi tunakwenda, na kama ilivyo sifa ya kazi zenu haihitaji maneno mengi sana, picha moja inaweza ikasema mambo mengi sana, tunaamini tutashirikiana kuijenga Tanzania tunayotaka, na sipo hapa kuwaombeni msifie niko hapa kuwaombeni mkosoe kadri mnavyoweza kwa sababu katika kukosoa mtasaidia kuipata Tanzania tunayoitaka, nyinyi taaluma yenu, kosoeni, shaurini na rekebesheni naamini mna nguvu sana, maana hata rais ni mtu anayetembelea sana mitandao.” Alisema.
Mtandao huo wa Bloggers Tanzania ambao umefanya mkutano mkuu wake wa kwanza, tangu uanzishwe mwaka jana 2015, umemthibitisha bw. Joachim Mushi, kuwa mwenyekiti wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kuchagua kamati mbalimbali mbatu kusaidiana na mwenyekiti na viongozi wenzake.Reactions:

0 comments:

Post a Comment