Monday, 19 December 2016

 MTU mmoja anahofiwa kufa, na wengine 14 kujeruhiwa vibaya baada ya gari moja jamii ya NOAH, lenye namba za usajili, T517 CDL, lililokuwa likisafiri kutoka Musoma kwenda Mbeya, kupinduka kwenye kijiji cha Nyagu, jimnbo la Mtera mkoani Dodoma kwenye barabara ya Iringa -Dodoma jioni ya Desemba 19, 2016.
Polisi wanasema, majeruhi walipelekwa kwenye kwenye kijiji jirani ili kupatiwa huduma wakati mipango ya kuwahamishia majeruhi kwenye hospitali ya rufaa ya Dodoma zikifanywa.
Dereva wa gari hilo, Bw.gari hilo lilikuwa likisafiri kutoka Musoma ambapo abiria wengi walikuwa wa familia moja, wakitoka kwenye sherehe kurejea nyumbani.
Aidha mashuhuda wa ajali hiyo wakiwemo wahariri wa vyombo vya habari wakiokuwa wakipita kwenye kijiji hicho kutoka ziara ya kikazi, waliliona gari hilo likiwa kwenye kasi likiacha njia na kupinduka mara kadhaa huku abiria wakirushwa kutoka madirishani wakiwemo watoto wanne, na mama mmoja mjamzito.
Waandishi hao walilazimika kusimamisha gari lao na kuanza shughuli za uokoaji ambapo walishiriki kuvunja mlango wa mbele wa gari upande wa abiria, ambako mama mjamzito alikuwa amebanwa.
Pichani chini ni juhudi mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na waandishi wa habari katika kuokoa majeruhi hao
Reactions:

0 comments:

Post a Comment