Monday, 12 December 2016


Wanamadrssa kutoka Mtendeni Mjini Unguja wakisoma Maulid ya Hom wakati wa sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)  sherehe hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 12, 2016 katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na  Sheikh Sherali Champsi Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipokea Zawadi ya Qaswida ya mwaka kutoka kwa Sheikh Sherali Champsi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Mashekhe mbali mbali na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakisimama kumswalia jana katika sherehe zilizofanyika katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifukiziwa Udi baada ya kutiliwa marashi wakati kumswalia mtume Muhamad (S.A.W) wakati sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa kiongozi huyo   sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Reactions:

0 comments:

Post a Comment