Wednesday, 7 December 2016

 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna wa Polisi, Mohammed Mpinga, akiwa amepanda moja kati ya bajaji mbili zilizotolewa kwa jeshi hilo, na Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), makao makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam, Desemba 7, 2016. kushoto ni Afisa Uhusiano wa TBL, Amanfa Walter ambaye ndiye aliyekabidhi bajajihizo kwa niaba ya TBL.
 Kamishna Mpinga akipokea funguo za bajaji kutoka kwa Amanda ikiwa ni ishara ya makabidhiano.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
KAMPUNI ya Bia Tanzania, (TBL), imekabidhi Bajaji mbili kwa Kikosi cha Usalama Barabarani ikiwa ni msada wa kampuni hiyo kuongeza nguvu juhudi za kusimamia usalama barabarni.
Akikabidhi bajaji hizo zenye thamani ya shilingi milioni 14 kwa Mkuuwa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna wa Polisi, Mohammed Mpinga makao makuuya kikosi hicho jijini Dar es Salaam leo Desemba 7, 2016, Afisa Uhusiano wa TBL, Amanda Walter amesema TBL imeona usalama barabarani ni kitu cha muhimu na ili kuimarishausimamizi mzuri wa usalama barabarani kampuni yake imeona iwaongezee nguvu jeshi lapoisi ii kuimarisha kazi hiyo.
Naye Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini, Kamishna wa Polisi, Mohammed Mpinga, aliishukuru TBL kwa msaada huo na kwamba unaongeza nguvu kwa kikosi chake kusimamia vizuri sheria za usalama barabarani.
“Msada huu umekuja wakati muafaka, hususan katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, ambao unahitaji usimamizi wa karibu zaidi na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa wananchi"
 Kamishna wa Polisi, Mohammed Mpinga, akizungumza wakati akipokea msada wa bajaji mbili kutoka Kampuni ya Bia Tanzania, 9TBL),makao makuu ya kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2016. Katikati ni Afisa Uhusiano wa TBL, Amanda Walter na kulia ni afisa wa polisi wa kikosi hicho, J.T Gwau
 Kamishna wa Polisi, Mohammed Mpinga, akizungumza wakati akipokea msada wa bajaji mbili kutoka Kampuni ya Bia Tanzania, 9TBL),makao makuu ya kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano wa TBL, Amanda Walter
 Afisa Uhusiano wa TBL, Amanda Walter, akizungumzia msada huo
 Maafisa wa kikosi cha usalama barabarani, waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano hayo
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani waliohudhuria hafla hiyo fupi
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani waliohudhuria hafla hiyo fupi
Reactions:

0 comments:

Post a Comment