Friday, 2 December 2016

 Mwakilishi wa benki ya NMB, Doris Kilale, (Kushoto), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, kwa Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika Desemba 2, 2016 kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI MAALUM


BENKI ya NMB imetoa shilingi Milioni 10, kwa Mtandao wa Wamiliki/Waendesha Mitandao ya Kijamii nchini Tanzania, (TBN), jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2016.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa benki hiyo, Doris Kilale alisema, NMB inatambua kuwa TBN ni wadau wakubwa na benki hiyo katika kuhabarisha umma, kwa hivyo benki imeona isaidie ili kufanikisha mkutano huo unaotarajiwa kuanza Jumatatu Desemba 5 jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi alisema, TBN ambayo  ilisajiliwa rasmi na Serikali Aprili mwaka jana, 2015 kwa kushirikiana na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii imeandaa semina kwa wanahabari hawa wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' wapatao 150 kutoka bara na visiwani.
Alisema mkutano huo ambao utaenda sambamba na mafunzo kwa wana TBN yatakayolenga kujenga uwezo juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato).Reactions:

0 comments:

Post a Comment