Friday, 23 December 2016


Na K-vis blog
MIGAPICHA mwandamizi wa kampuni ya The guardian limited, Mpoki Bukuku amefariki dunia mapema leo Desemba 23, 2016 kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, alikopelekwa baada ya kupata ajali Uusiku wa alhamisi Desemba 22, 2016.
Kwa mujibu wa mpiga picha mkuu wa kampuni hiyo, Selemani Mpochi, Mpoki alipata jaili hiyo wakati akitoka kazini kuelekea nyumbani kwake, na alipelekwa hospitali ya taifa muhimbili kwa ajili ya matibabu na ilipofika majira ya asubuhi leo, alipoteza maisha.
“huyu bawa nilimuacha kazini, na taarifa nizliopewa, majira ya saa tatu hivi usiku, wakati akivuka barabara ya bagamoyo eneo la menge, aligongwa na gari na kuvunjika miguu. mkono na mbavu, pia aliheruhiwa kichwani.”alisema Mpochi
Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwake Tabata- kimanga jijini Dar es salaam.
Mpoki Bukuku ambaye pia alijulikana kama “sumo” kutokana na mwili wake mkubwa, aliwahi kuzifanyia kazi kampuni za Business Times/majira, kabla ya kujiunga na kampuni ya Mwananchi Communication, ambako alikuwa mpiga picha mkuu.
Marehemu ameacha mke na watoto.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi amin.
Tumepoteza nguzo katika tasnia ya habari

Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Ltd, kuhusu kifo cha Mpoki Bukuiu.
 Leo, kama ilivyo kwa wengine wengi, nimepokea kwa mshtuko mkubwa na kutoamini, kuhusiana na kifo cha ghafla cha mmoja wa wapigapicha waandamizi wa The Guardian Limited, Bw. Mpoki Bukuku (44), aliyefariki asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa familia yake, wamempoteza baba, mume na zaidi ya yote rafiki wa kweli, lakini kwetu sisi The Guardian Limited, tumempoteza pia rafiki wa kweli na nguzo katika tasnia ya uandishi wa habari.

  Bukuku alikuwa ni mwanadamu tu kama ilivyo kwa yeyote kati yetu, lakini katika uandishi wa habari, alikuwa ni mtu aliyeipenda fani yake na hakuogopa kupambana alimradi apate habari nzuri. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kuna wakati kiu yake ya kupata habari nzuri kuliko wengine wote ilimuweka matatani.

Wale wanaoelewa uandishi wa habari wa picha watabaini kwamba ujasiri na kuipenda kazi ni sifa kuu mbili za kila mpigapicha ili kupata habari nzuri na yenye nguvu. Bukuku alikuwa na sifa zote hizo mbili. Alikuwa shujaa na mwenye mapenzi na kazi yake hasa wakati akifuatilia habari kubwa kokote kule katika nchi hii.

 Alipigwa na hata kuteswa na maadui wa uhuru wa vyombo vya habari, lakini bado mahaba yake katika kufanikisha habari bora hayakuzimwa. Alikuwa ni mwandishi wa habari siyo kwa bahati mbaya, bali ni kwa kuchagua na ndiyo maana alikuwa na mapenzi wakati akitimiza wajibu wake wa kutekeleza kazi mbalimbali za kihabari alizopangiwa na wahariri wake.

Bukuku amemaliza safari yake duniani, kimwili hayuko nasi lakini kiroho na kiuweledi, mara zote atakuwa nasi daima.

Sisi katika Kampuni ya The Guardian Limited tunaungana na famila, ndugu na marafiki katika kippindi hiki kigumu, kuombeleza msiba wa mtu ambaye tumekuwa tukifanya naye kazi kwa miaka mingi. Kampuni itaiunga mkono kwa ukamilifu familia ya marehemu Bukuku.

Kwa niaba ya wafanyakazi wote wa The Guardian Limited, kwa heshima kubwa natoa salamu zangu za rambirambi kwa mjane wa Bukuku, Lucy, watoto na wadau wote wa tasnia ya habari nchini Tanzania, kwa kifo cha ghafla na kushtua cha mmoja wetu.Richard Mgamba

Mkurugenzi Mtendaji,

The Guardian Limited

Desemba 23, 2016
Reactions:

0 comments:

Post a Comment