Friday, 30 December 2016


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea  zawadi za pampers ambazo zitatumika kwa watoto waliolazwa kutoka kwa Mary Mabano ambaye mwaka 2008 alifanyiwa  upasuaji na madaktari wa Taasisi hiyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha  damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja. Siku ya jana tarehe 28/12/2016 Mary alikuwa anatimiza umri wa miaka 23 na aliamua kusherehekea siku hiyo na wagonjwa wa moyo.


Mary Mabano akimlisha keki Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo  Tulizo Shemu Sanga ambaye  ndiye daktari anaendelea kumtibu  Mary. Mwaka 2008 Mary alifanyiwa    upasuaji wa moyo na  kuwekewa Valve moja kwa kuwa  Valve yake ya kuzaliwa nayo ilikuwa na tatizo la kutokupitisha damu vizuri.


Mary Mabano akimlisha keki Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo.


Mary Mabano akimlisha keki mgonjwa wa Moyo Nasra Hamis  ambaye amefanyiwa upasuaji na kuwekewa Valve ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo wake.


Mary Mabano akimkabidhi Afisa Muuguzi Msaidizi ambaye pia ni msimamizi wa wodi namba tatu (3) iliyoko Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Rogers Kibula zawadi ya sabuni ya unga ya  kufulia ambayo itatumika kwa ajili ya  usafi wakati wa sherehe yake ya  kutimiza miaka 23 iliyofanyia jana katika Taasisi hiyo. Mary alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na wagonjwa wa Moyo kwa kuwa hata yeye mwaka 2008 alifanyiwa  upasuaji wa moyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha  damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja.


Mary Mabano akikata keki wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku Madaktari Bingwa wa moyo, wauguzi, ndugu na jamaa wakishuhudia.Madaktari Bingwa wa Moyo, Wauguzi , wagonjwa wa Moyo, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa Mary Mabano ambaye aliyesherehea siku hiyo na wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Wa tano kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.

(PICHA NA ANNA NKINDA – JKCI)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment