Friday, 30 December 2016

Rais wa Russia, Vladimir Putin


MAREKANI imetoa masaa 72 kwa wanadiplomasia 35 wa Russia kuondoka nchini humo ikiwatuhumu kuingilia uchaguzio mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Novemba pita.
Hatua hiyo inakwenda sambamba na kufungwa kwa majengo mawili yanayotumiwa na Russia kwa masuala ya kijasusi
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema, hatua hiyo dhidi ya wanadiplomasia hao inafuatia ukiukwaji wa majukumu yao, kwa kufanya shambulio la kimtandao, (cyber attack), dhidi ya chama cha Democrat na aliyekuwa mgombea wake wa kiti cha Rais, Bibi Hilary Clinton.
Hata hivyo Russia imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na tuhuma hizo na kuita tuhuma hizo hazina ushahidi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imetangaza wanadiplomasia 35 wa Russia kutoka mji mkuu Washington na ubalozi mdogo wa Russia mjini San Francisco kuwa watu hao na familia zao hawatambuliwi na kupewa saa 72 wawe wamefungasha virago na kuondoka nchini humo.
Kremlin imesema haitalipiza kisasi na haina mpango wa kuwafurusha wanadiplomasia 31 wa Marekani walio kwenye miji ya Moscow na

Saint Petersburg

Reactions:

0 comments:

Post a Comment