Monday, 26 December 2016

Waziri wa habari, utamàduni, sanaa na michezo, Ñape Nnauye, akitoa heshma za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwandamizi wa The Guardian, Mpoki Bukuku wakati wa kuaga mwili wa marehemu kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya wazazi, Tabata jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2016. Marehemu Mpoki ambaye pia alijulikana kwa jina LA utani SUMO, kutokana na umbile lake la miraba minne, alifariki Ijumaa wakati akipatiwa matibabu kwenye taasisi ya mifupa (MOI), baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara ya Bagamoyo eneo LA Mwenge, Alhamisi usiku. Marehemu ambaye ameacha mke na watoto watatu na anatarajiwa kuzikwa Msalato, Dodoma Jumanne Desemba 27, 2016.
Waziri Nape, akisalikiana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Kushoto ni mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu kuelekea eneo la kutoa heshima za.mwisho
Wapiga picha wakibadilishana mawazo, kutoka kushoto, Badi John(The Guardian), Zainul Mzige(Mo Blog, Khalfan Said(K-VIS Blog. na Muhidin Issa Michuzi(Mpiga picha wa Rais).
Mpiga picha Mkuu wa The Guardian Ltd, Selemani Mpochi(kushoto), akisalimiqna na Freddy Maro, wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mwalimu Nyerere, wengine pichani kutoka kushoto ni Muhidin Issa Michuzi, mpiga picha wa Rais, Badi John(The Guardian) na Khalfan Said, wa K-VIS blog.
Mpiga picha Mkuu wa The Guardian Ltd, Selemani Mpochi, akizungumza.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment