Tuesday, 6 December 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, impelekee vielelezo vya namna Faru aliyepewa jina la JOHN kuhamishwa kutoka kwenye hifadhi hiyo na kupelekwa kwenye hoteli moja mwaka 2015 na sasa inaelezwa kuwa amekufa. Waziri mkuu pamoja na mambo mengine, ameutaka uongozi wa hifadhi hiyo kama unadai eti Faru JOHN keshakufa, wampelekee na kielelezo cha pembe zake. Pichani Waziri Mkuu akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Baadhi ya watumishi wa Mamlka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016
Reactions:

0 comments:

Post a Comment