Friday, 23 December 2016


Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akisisitiza jambo kwa watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For Orphanage Kigamboni (hawapo pichani) mapema hii leo wakati wa kupokea msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto hao, kushoto ni Mlezi wa kituo hicho Hajjat Zubeda  na kulia ni Mkiurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uhuru Music (T) Ltd. Bw. Maneno Sanga.


Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Amani Foundation For Orphanage Kigamboni Hajjat Zubeda akitoa historia fupi ya kituo hicho wakati wa kupokea msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile na kulia mwisho ni Mkiurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uhuru Music (T) Ltd. Bw. Maneno Sanga.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uhuru Music (T) Ltd. Bw. Maneno Sanga akimvisha shati moja ya watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For Orphanage mapema hii leo wakati wa wakitoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uhuru Music (T) Ltd. Bw. Maneno Sanga akisisitiza jambo kwa watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For Orphanage Kigamboni (hawapo pichani) mapema hii leo wakati wa wakitoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Dege Stationery & general Supply Bw. Michael Muywanga akiongea na watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For Orphanage Kigamboni (hawapo pichani) mapema hii leo wakati wa wakitoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.


Baadhi ya wageni wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For Orphanage Kigamboni mapema hii leo wakati wa wakitoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.(PICHA ZOTE NA ELIPHACE MARWA – MAELEZO)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment