Monday, 5 December 2016


Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogo wadogo, Joyce Malai, wakionyesha kadi inayoonyesha uzinduzi wa ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Uzinduzi huo ulifanyika Desemba 5, 2016 makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU.


BancABC ya jijini Dar es Salaam, leo Desemba 5, 2016, imezindua ofa ya riba hadi asilimia 16% kwa mteja anayefungua akaunti ya amana ya muda maalum, (Fixed Account), msimu huu wa sikuku.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jingo la Uhuru Hights jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa benki hiyo, Bi. Joyce Malai, alisema, riba hiyo itatolewa kwa mwaka na mteja atalipwa riba papo kwa papo ikiwa ni zawadi yake ya msimu wa sikukuu.

“Hii ni ofa bora kuliko zote kwenye soko kwa sasa na tunataka kuwashawishi wateja wetu na hata wale wasiokuwa na akaunti kwetu kutumia fursa ya ofa hii ya msimu wa sikukuu.” Alifafanua.

Bi. Malai alisema, “benki inathamini jinsi wateja wetu wanavyotuunga mkono na hiyo ndiyo sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe katika msimu huu wa sikukuu.”

Alisema mteja anaweza kufika tawi lolote la benki hiyo lililoko Uhuru, Quality Centre, Kariakoo jijini Dar es Salaam na mkoani Arusha ili kufungua akaunti hiyo ambapo riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kumpa mteja uhuru wa kutumia kwa ajili ya kufanya manunuzi binafsi kama apendavyo.

“Tunajua wakati huu, watu wengi wanajiandaa kulipa ada, kununua mahitaji mbaimbali kwa ajili ya sikuu, na wengine kwenda kupumzika kwenye maeneo mbaimbali, hivyo wakati unasubiri kufanya mambo hayo ni vema fedha zako ukazileta hapa benki na kuzitunza na muda wa kufanya hayo matumizi ukifika, basi unakuja kuzichukua na faida.” Aliongeza Mkuu wa Masoko na Hazina wa benki hiyo, Bw.Barton Mwasamengo.


Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogowadogo, Joyce Malai, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, kuzindua ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Uzinduzi huo ulifanyika Desemba 5, 2016 makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogowadogo, Joyce Malai
 Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo,
 Waandishi wa habari
 Bi.Upendo Nkini(kulia), akiwakaribisha maafisa hao tayari kuzungumza na waandishi wa habari


Reactions:

0 comments:

Post a Comment