Tuesday, 6 December 2016Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wawili wa JWTZ kuwa Meja Jenerali kuanzia tarehe 03 Disemba 2016.Maafisa Wakuu hao ni;
Brigedia Jenerali George William Ingram ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga, (pichani kulia), na Brigedia Jenerali Michael Wambura Isamuhyo, (pichani kushoto),  ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Taarifa ya Makao Makuu ya JWTZ iliyotolewa jana Desemba 6 imesema, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu anawapongeza na kuwatakia kheri katika vyeo vyao vipya.
Reactions:

1 comments:

Post a Comment