Saturday, 24 December 2016

 KWA wasafiri wengi wanaotumia usafiriwa barabara, hujipatia fursa ya kufanya manunuzi ya mahitaji yao ya nyumbani, iwe mazao ya jamii ya mbogamboga, viazi, mahindi na hata wanyama kama mbuzi na kuku, ama kwa hakika ni fursa nzuri wanayoipata kununua mazao ambayo bado hayajachukua muda mrefu tangu kuvunwa tena kwa bei nafuu sana. Miongoni mwa mazao yanayopatikana kwa wingi ni pamoja na nyanya na vitunguu, lakini jambo la kusikitisha, pengine kutokana na kutokuwepo kwa mipangom thabiti ya kuwainua wakulima hawa, mazao yao huyauza kwa bei ya "kutupa"ni ndio maana wasafiri huchangamkia fursa hiyo kununua bidhaa hizo kwa "fujo" tena wengine hunogew ahadi kuachwa na vyombo vya usafiri kama ni abiria wa bus.


 Mchuuzi wa mahindi akiwa katika harakati za kusaka wateja ambao ni abiria
 Abiria akionyeshwa bidhaa na wachuuzi
 Wanendesha magari wakiwa eneo la biashaya ya mazao ya matunda na mbogamboga barabara ya Msata Bagamoyo kwenye daraja la Ruvu
 Mchuuzi wa kuku akiwa amebeba kuku zake tayari kwa kuuza tena bei poa ya shilingi kati ya elfu 10 na elfu 15
 Akiwa na tabasamu, mchuuzi huyu wa nyanya, tayari ameliona gari linakaribia kuegesha ili kununua bidhaa zao
 Wachuuzi wa mazao mbalimbali wakiwa wanawaonyesha abiria bidhaa zao
 Mchuuzi wa nyanya akisubiri wateja
Huyu ni abiria akikimbilia basi baada ya kuachwa, kutokana na "kunogewa" na manunuzi ya biadhaa zinazouzwa kandokando ya barabara kuu ya Dar es Salaam, Dodoma eneo la katikati ya Gairo na Dumila mkoani Morogoro
Reactions:

0 comments:

Post a Comment