Tuesday, 8 November 2016NA K-VIS MEDAI/MASHIRIKAYAHABARI
MGOMBEA kiti chaRais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, Bibi. Hillary Clinton, anaongoza kwenye uchaguzi huo wakati Wamarekani wameanza kupiga kura leo Novemba 8, 2016, hata hivyo mpinzani wake, Bw. Donald Trump,wa chama cha Republican anamfuatia kwa karibu sana
Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Kimataifa, matokeo mapya kabisa yanaonyesha Bibi Clinton yuko mbele kwa asilimia 45.9% wakati mpinzani wake Bw. Donald Trump wa Republican ana asilimia 42.8%.
Matokeo hayo yanekuja siku moja tu baada ya Shirikala Upelelezi la Marekani FBI, kumsafisha Bibi Clinton kutokana na tuhuma mpya za email zaidi ya 600,000, zilizokutwa kwenye anuani yake binafsi ya barua pepe kuwa hazikuwab na madhara yoyote katika usalama wa taifa hilo kubwa kabisa Duniani.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment