Tuesday, 1 November 2016

 Dusntan Tido Mhando, Mkuruhenzi wa Azam TV
 K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MTANGAZAJI mkongwe nchini Dunstan Tido Mhando, “atamkabili” Rais John Pombe Magufuli, katika mahojiano ya moja kwa moja yatakayofanyika Novemba 4, 2016 kuanzia saa 4 asubuhi.
Tido ambaye ni Mkurugenzi wa Azam TV, na mwenye uzoefu wa karibu miaka 40 katika utangazaji, atashirikiana na Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba kwenye mahojiano hayo ambayo pia yatashirikisha wahariri wengine wa vyombo vya habari na kupeperushwa moja kwa moja kupitia runinga.
Tido Muhando ambaye awali alikuwa nchini Uingereza akifanyia kazi Shirika la Habari la Uingereza BBC, kama mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, anauzoefu mkubwa wa kufanya mahojiano “interview” na marais mbalimbali barani Afrika.
Miongoni mwa Maris aliowahi kuwafanyia mahojiano ni pamoja na hayati Rais Laurent Kabila wa DRC, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na Hayati Mwalimu Nyerere
Tido anasifika kwa ufundi wa kuuliza maswali yenye mantiki na bila woga. Kwa mujibu wa wachambuziwa masuala ya habari, hii itakuwa fursa nzuri ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuelezea tathmini yake ya utawala katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani Novemba iliyopita.
Akihojiwa na mtangazaji mwingine gwiji wa Azam TV, Charles Hillary kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku Oktoba 31, 2016, Tido alsema, anatarajia mahojiano hayo yatakuwa mazuri. “Baada ya jitihada nyingi tulizofanya za kufanya mahojiano na Mheshimiwa Rais Magufuli kugonga mwamba mara kadhaa, safari hii Ikulu imetukubalia na ninahakika yatakuwa mahojiano mazuri na motomoto,” Alisema Tido.

 Rais Dkt. John Pomba Magufuli, akiwa amekamata ngao na mkuki siku alipoapishwa kushika madaraka yakuiongoza Tanzania Novemba 2016.
 Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba
 Tido akifanya mahojiano na Rais mstaafu Jakaya Kikwete
Tido akifanya mahojiano na Hayati Laurent Kabila, aliyekuwa Rais wa DRC. Inaelezwa kuwa mahojiano haya ndiyo yalikuwa ya mwisho kwa rais huyo kuhojiwa na vyombo vya habari hadi mauti yalipomkuta
Reactions:

0 comments:

Post a Comment