Tuesday, 1 November 2016

 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (mwenye mpama), "akikata kiu" kwenye nyumba moja, wakati wa ziara yake ya nyumbakwa nyumba kuhamasisha wananchi kuondokana na umasikini kupitia operesheni aliyoanzisha ya "Vumbua Utajiri".RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, ameanza kampenio ya nyumba kwa nhyumba aliyoipa jina la “Vumbua utajiri” ikiwa na lengo la kuhamasisha umma kuondokana na umasikinikwa kutumia mazingira yanayowazunguka.
Ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye anaanza na wengine wanafuata kwenye operesheni hiyo ya “Wealth creation), Rais Museveni alichapisha picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa Facebook Oktoba 31, 2016 akiwa kwenye Kawaumu wilaya ya Luweero, ambapo alionekana akikokota baiskeli iliyokuwa na dumu, akitoka kuchota maji ili akamwagilie shamba lake la kahawa na ndizi.
Katika maneno yake aliyochapisha kwenye ukurasahuo Rais alisema “Leo ni sikuya tatau ya operesheni yangu ya Uvumbuzi wa utajiri hapa Luweero, Asubuhi hii nimechota maji na kuyabeba kwenye baskeli yangu kwa nia ya kuonyesha umwagiliaji kwenye shamba la Kahawa na Migomba ambayo nimepanda kwenye ekari 24 hivi karibuni nilizopewa na serikali hapa Luweero. Nitaendelea na kampeni yangu ya mlango kwa mlango kuhamasisha na kusisitiza juu ya operesheni “Vumbua Utajiri.”Alisema Rais Museveni kwenye ukurasa huo wa Facebook.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment