Thursday, 10 November 2016

 Askari polisi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Samwel Sitta, Mzee wa "Speed na Viwango", ulipowasili alasiri hii kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ukitokea nchini Ujerumani leo Novemba 10, 2016. Marehemu Sitta ambaye alikuwa Spika wa bunge la 9 la serikali ya awamu ya nne, alijizolea umaarugu mkubwa miongoni mwa watanzania, kutokana na jinsi alivyoliendesha bunge hilo, ambapo liliibua kashfa mbalimbali.
Spika wa bunge job Ndugai umetangaza utaratibu wa kuaga mwili wa mwanasiasa huyo mkongwe nchini, ambapo shughuli nzima itafanyika kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma. Taarifa kamili ya spika inapatikana hapo chini.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, (kulia), akimfariji mjane wa marehemu, Mama Margareth Sitta, alipowasili na mwili wa mumewe Samel Sitta kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2016.Reactions:

0 comments:

Post a Comment