Thursday, 10 November 2016


NA K-VIS MEDIA
MWANASIASA na Mwanamichezo, Mh. Hafidh Ali Tahir, amefariki dunia kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma mapema leo saa 9 alfajiri Novemba 11, 2016.
“Mh. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tannzaia  anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya General mkoani Dodoma,” Taarifa ya bunge imesema. Haikuelezwa ni maradhi gani yalikuwa yakimsumbua.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Mhe Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.
Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na waheshimiwa wabunge katika vikao vya bunge, taarifa hiyo ya bunge ilifafanua.

Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 Dimani Mjini Magharibi na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1972-1978) na amekuwa Mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.
Kwa wale wanaofuatilia masuala ya soka, watakumbuka kuwa marehemu Hafidh Ali Tahir, alikuwa Mtanzania wa kwanza kuwa refa wa kimataifa anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA.

Marehemu Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir ameacha Mke mmoja na Watoto Saba

Mh. Hafidh Ali Tahir, akiwa na naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais, (Muungano na Mazingira), Mh. Luhaga Mpina, (kulia), akizungumza jambo wakati wa ziara ya Mh. Mpina kukagua mazingira jimbo la Dimani.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment