Tuesday, 1 November 2016


Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 29/- Mkazi wa Shangarai mkoani Arusha, Kaungame Menas(kulia)alizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa M-bet. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 1, 2016. Katikati ni Msemaji wa M bet, Godluck Wambura.

NA MWANDISHI WETU
Mkazi wa Arusha Mjini, Kaungame Menas Soko mwenye umri wa miaka 28 ameibuka mshindi baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi kupitia Kampuni ya m-Bet na kujishindia Shilingi Milioni 29/-.
Kaungame amekabidhiwa fedha zake leo katika hafla  fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za m-Bet
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kabba alisema kuwa Kaungame alifanikiwa kuzoa kitita hich baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 15 za ligi ya Ulaya kwa mtindo wa mcheza kawaida.
“Tunafarijika kumkabidhi Kaungame Menas  kitita hicho cha Sh milioni 29/- akiwa ndiye mshindi wa m-Bet ambapo atapata Sh milioni 29/- kabla ya makato ya kodi,” alisema Kabba.
Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe.
Naye Mshindi huyo, Kaungame Menas  amewashauri watanzania wote wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya m-Bet .

"Nashukuru sana m-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto yangu ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi", alisema Mena
Kuhusu m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima
“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Perfect 12 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-Bet,” alisema Kaba.Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba(kushoto)na Msemaji wa M bet,Godluck Wambura(kulia)wakimshuhudia mshindi wa shilingi milioni 29/- Mkazi wa shangarai mkoani Arusha, Kaungame Menas(katikati)akisaini fomu kwa ajili ya malipo ya fedha zake alizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa M bet,wakati wa hafla ya kumkabidhi hundi yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment