Tuesday, 15 November 2016


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionyesha hati ya muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2016, baada ya kusaini hati hiyo  katika hafla iliyofanyika leo Novemba 15, 2016 Ikulu Mjini Unguja, ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)
NA K-VIS BLOG
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, ametia saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, uliopitishwa hivi karibuni na Baraza la Wawakilishi na kusema, rasilimali hizo ni mali ya Wazanzibari.
Akijibu swali la mwandishi wa habari, Munir Zacharia aliyetaka kujua kama Rasilimali hizo endapo zitapatikana visiwani humo, yawezekana zikachimbwa huko na kupelekwa Bara (Tanzania bara)?, “Mafuta na gesi yakipatikana Zanzibar, ni mali ya Wazanzibari, kama wenzetu wa Tanzania Bara, wakiyahitaji, tutawauzia kama ilivyo kwa wengine, barrel, (pipa), moja dola 70, haya,” Alijibu Dkt. Shein katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali yake, wakiwemo, Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Mwanasheria Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju.
Hafla hiyo iliyokuwa ikipeperushwa moja kwa moja na Televisheni ya Zanzibar, (ZBC), ilifanyika Ikulu ya Zanzibar leo Novemba 15, ambapo baada ya Rais kusaini muswada huo na kuwa sheria, alitoa nafasi ya kuulizwa maswali mawili tu.
Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa ni pamoja na lile la mtangazaji wa ITV-Zanzibar, Farouk Karim ambaye aliuliza, kuwa wapo wanasheria waliotahadharisha kuwa, Rais wa Zanzibara sisaini muswada huo kwa vile atakuwa amekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kwa mujibu wa Karim, ni swala la Muungano.
Akijibu swali hilo, Rais wa Zanzibar alisisitiza kuwa , hajafunja sheria wala katiba, na kwamba alichofanya kimo ndani ya katiba ya Zanzibar na kwamba, na kuwashauri wanasheria hao kusoma vifungu vyote na sio nusu nusu.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafla hiyo.

Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Sospiter Muhongo,(kushoto), akiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe, Zubeir Ali Maulid (kulia) wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, Ikulu ya Zanzibar Novemba 15, 2016
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali  wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali  wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
 Viongozi kutoka kushoto Kadhi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Sheihk Khamis Haji,Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Radhid Ali Juma,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Naibu waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe,Juma Makungu Juma  wakiwa katika  Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa  leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Ikulu Mjini Unguja

Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Reactions:

0 comments:

Post a Comment