Tuesday, 8 November 2016NA K-VIS MEDIA
WAZIRI wa zamani Bw. Joseph Mungai, (pichani), amefariki dunia jioni hii ya Novemba 8, 2016.
Hospitali ya taifa Muhimbili, (MNH), imethibitisha kupokea mwili wa marehemu kupitia kitengo chake cha wagonjwa wa dharura ambapo hospitali hiyo ilithibitisha kifo chake.
“Tumepokea mwili wa marehemuJoseph Mungai kupitia idara yetu ya magonjwa ya dharura na kuthibitisha kifo saa 11;20 jioni hii ya Novemba 8, 2016.” Mkuu wa kitengo cha Mahusiano cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), Aminieli Aligaesha amenukuliwa akithibitisha taarifa hizo.
Joseph Mungai, alikuwa waziri tangu serikali ya awamu ya kwanza, na zilizofuatia kabla ya kukihama chama cha mapinduzi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita 2015 ambapo yeye na mkewe walijiunga na CHADEMA.


Joseph Mungai akihutubia mkutano wa hadhara wa CHADEMA, baada ya kutangaza kujiondoa CCM
Reactions:

0 comments:

Post a Comment