Wednesday, 2 November 2016


 Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (Wa kwanza kushoto ) akizungumza na uongozi wa East Afrika Televisheni  na East Afrika Radio  alipotembelea vituo hivyo  Novemba 2 mwaka huu  Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa vipindi vya EATV Bi Lydia Igarabuza.

Mkuu wa vipindi vya East Afrika Televisheni  Bi Lydia Igarabuza (wa kwana kulia) akimueleza jambo Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho Novemba 2  mwaka huu Jijini Dar es Salaam

Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji  wa EATV  Na EA Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2  mwaka huu Jijini Dar es Salaam.Bodi ya Filamu yaendelea  kutoa elimu kwa wasanii kuhusu kutengeneza filamu bora.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo amewashauri  wasanii wa filamu nchini  kujiendeleza kielimu ili kuongeza  weledi na kutengeneza filamu zenye ubora.
Akiongea na   uongozi wa Kituo cha  Radio na Televisheni  cha East Afrika  leo   Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa chombo hicho  kina nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa wasanii hususani namna ya kuandaa  Filamu zenye  bora kwa kuwa wako mstari wa mbele katika kuonyesha kazi za  tasnia hiyo. 
“Kituo chenu kina nafasi kubwa zaidi ya kushawishi wasanii kutengeneza filamu bora kwa kuwa  mmekuwa mkiwapatia fursa ya kutangaza filamu hizo pamoja na kuzionyesha ndani na nje ya nchi hivyo ni muhimu kuwakumbusha  kuzingatia ubora wa filamu .”Alisema Bibi Joyce.
Aidha ameongeza kuwa vyombo vya Habari ni nguzo muhimu katika kuendeleza tasnia ya filamu  hapa nchini hivyo ni budi kwa wasanii kuhakikisha wanatengeneza Filamu bora ambazo zitapata nafasi ya kuonyeshwa katika vyombo hivyo  kwa maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Naye  Mkuu wa vipindi vya televisheni wa   East Afrika Bi Lydia Igarabuza  ameipongeza Bodi ya Filamu kwa  kufanya maboresho katika tasnia ya Filamu nchini na kuishauri kutoa elimu zaidi kwa wasanii  katika  kufuata Sheria ya Filamu na michezo ya kuigiza kabla ya kutengeneza filamu zao.
“Naipongeza Bodi ya Filamu kwa juhudi mnazofanya katika kuboresha tasnia  hii  na msichoke  kutoa elimu hiyo kwani wasanii wetu bado wanahitaji elimu ya filamu na sheria zake kwa ujumla.Alisema Bi Lydia.
Bodi ya Filamu imejidhatiti katika kuhakikisha tasnia ya Filamu inakuwa kwa kutengeneza bidhaa bora ambapo imekuwa  ikitoa mafunzo  kuwajengea uwezo wanatasnia hao  .
Reactions:

0 comments:

Post a Comment