Sunday, 14 August 2016NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
RAIS wa pili na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Serikali ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, (96), amefariki dunia leo Agosti 14, 2016.
Mwinyi ambaye alikuwa akiishi Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es Salaam, tangu patokee “mchafuko wa hali ya hewa” kisiwani Zanzibar, alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Hayati Jumbe alianza kuitawala Zanzibar mnamo Aprili 11, 1972 mara baada ya kuuawa Rais wa Kwanza wa visiwa hivyo, Hayati Mzee Abeid Aman Karume Aprili 7, 1972.
Mzee Jumbe alitawala visiwa hivyo tangu wakati huo hadi Januari 30, 1984 alipojiuzulu kufuatia msimamo wake wa kutaka mabadiliko katika mfumo wa Muungano wa baina ya Zanzibar na Tanzania bara.
Mzee Mwinyi alizaliwa Juni 14, 1920) kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya utawala wa Rais wa kwanza wa Tanzania Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Pia Mzee Karume kwa mujibu wa utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, kwa madaraka yake ya kuwa Rais wa Zanzibar pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, (Zanzibar)
Mwenyezimungu ailaze roho yake mahala pema peponi AMIN
Reactions:

0 comments:

Post a Comment