Wednesday, 31 August 2016RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa, (pichani) kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Directorate of Presidential Communication - DPC).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo.

Kabla ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015.
Awalikabla ya kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alikuwa mtangazaji wa Televisheniya Taifa TBC mkoani Ruvuma

 Gerson Msigwa akiwa na Mke wake Catherine Nyoni kwenye moja ya hafla
 Akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Msigwa (wapili kulia), akimsaidia mtangazaji wa ITV, kuripoti wakati wa ziara ya Rais John Pombe Magufuli hivi karibuni wilayani Chato
Msigwa wakati akiwa mtangazaji wa TBC, akifanya maoja ya mahojiano
Reactions:

0 comments:

Post a Comment