Saturday, 14 November 2015

Mbwana Samatta (kushoto), na mwenzake Thomas Ulimwengu, wakishangilia bao


Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya soka ya taifa Taifa Stars, Mbwana Samata, amepachika bao la pili kwenye dakika ya 54 na hivyo kuifanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya Algeria kwenye pambano linaloendelea kuchezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.  Elias Maguri, aipatia bao la kuongoza timu hiyo dhidi ya Algeria kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, dakika ya 43  leo Novemba 14, 2015
Stars inachauna na Algeria katika pambano la kwanza la kuwania kuingia raundi ya pili ya michuano ya kuwaniankucheza fainali za kombe la Dunia. Stars inatafuta nafasi ya kushiriki fainali za kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika nchini Urusi. Timu ziko mapumziko kwa sasa. Hata hivyo Stars ilishindwa kulinda mabao hayo na hivyo kuwapa mwanya Walgeria kusawazisha mabao hayo 2 na matokeo hadi sasa ni 2-2
Reactions:

0 comments:

Post a Comment