Saturday, 14 November 2015

 Alphonce Mawazo enzi za uhai wake
Na K-Vis Media
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Geita, Bw. Alphonce Mawazo, ameuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa shoka na watu wasiojulikana mapema leo Jumamosi Novemba 14, 2015.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na polisi zinasema, Mawazo, alivamiwa na kundi la watu wakati akiwa kwenye kampeni za udiwani kwenye eneo moja la vijijini huko mkoani Geita na kuanza kumshambulia kwa mapanga na hata alipokimbizwa hospitalini kwa matibabu, tayari mauti yalikwisha mkuta.
Mawazo atakumbukwa na wana Chadema kutokana na umahiri wake katika ushawishi wa kisiasa ambapo alijijengea heshima kubwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini.
Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kadri tutakavyozipokea.


Alphonce Mawazo alipofikishwa hospitalini mapema leo Novemba 14, 2015 baada ya kujeruhiwa na mabanga, ambapo baadaye alifariki dunia
Reactions:

0 comments:

Post a Comment