Friday, 28 August 2015

 Msanii wa Filamu Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya  baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
 JK akitoa hotuba wakati wa hafla hiyo

Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM. Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakiongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mhe.Alpha Oumar Konare ambaye ni msuluhishi wa Umoja wa Afrika(AU) katika mgogoro wa Sudan ya Kusini Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Mbali na majadiliano yaliyohusu vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa changa la Sudan ya Kusini Bwana Konare ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Mali(1992-2002) na mwenyekiti mstaafu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika alimweleza Rais Kikwete umuhimu wa kutumia Kiswahili katika mikutano ya Umoja wa Afrika.(Picha na Freddy Maro)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment