Saturday, 18 July 2015

 Vijana wa Kundi  la 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, washangilia baada kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWA.
KUNDI la vijana la 4U Movement, lililokuwa likimiuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Edward Lowassa, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM, limetangaza leo Jumamosi Julai 18, 2015, kuunga mkono vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, almaarufu kama UKAWA.
Tangazo hilo lilitolewa na Mratibu wa Taifa wa Kundi hilo, Hemed Ali, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo mchana.
Baadhi ya wanachama wa kundi hilo walikuwepo wakati kiongozi wao anatangaza msimamo huo mpya.
Sababu za kuunga mkono UKAWA, zimeelezwa na kiongozi huyo kuwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, ambapo walidai kuwa katiba ya CCM haikufuatwa na baadhi ya makada wa chama hicho, akiwemo Mh. Lowassa, hawakutendewa haki.


 Kiongozi wa Kundi  Vijana wa 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Hemed Ali akizungumza na waandishi wa habari jjini Dar es Salaam leo Julai 18, 2015 kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWAReactions:

1 comments:

Post a Comment