Saturday, 18 July 2015

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitoa Mkono wa Iddi kwa wananchi mbali mbali waliofika  viwanja vya Ikulu mjini Unguja leo Jumamoasi Julai 18, 2015, katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri. Waislamu wa Tanzania wameungana na wenzao kote Duniani kusherehekea sikukuu hii baada ya kutekeleza ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
 Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa kwenye sala ya Eid, kwenye uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma, Julai 17, 2015
 Baadhi ya Viongozi na wananchi wakiwa katika swala ya Suna ya Idd el Fitri iliyoswaliwa kitaifa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Salum Mwalimu Juma aliongoza Swala hiyo
 Baadhi ya Viongozi na wananchi wakiwa katika swala ya Suna ya Idd el Fitri iliyoswaliwa kitaifa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Salum Mwalimu Juma aliongoza Swala hiyo


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein(wa pili kulia) akijumuika na Viongozi na waislamu mbali mbali katika swala ya Suna ya Idd el Fitri iliyoswaliwa kitaifa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za Baraza la Iddi el Fitri zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama bwawani Hotel Mjini Unguja,
 Baadhi ya Wake wa Viongozi na wananchi mbali mbali wakisikiliza hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein aliyoitoa leo katika kusherehekea Sikukuu ya Idd elFitri katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja


 Waislamu mkoani Dodoma wakiwa kwenye sala ya Eid


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wapili kushoto), akishiriki swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri na waumini wa Dini ya Kiislamu iliyofanyika Kitaifa wa Mkoani  Geita  leo Julai 18, 2015
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Baadhi ya Viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, (BAKWATA) na wananchi katika swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi  Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18,

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa dini ya Kisslamu wakati wa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally, baada ya kumalizika kwa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi, Kalangalala, mkoani Geita, leo Julai 18, 2015
 Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally, akitoa hotuba wakati wa sala hiyo
 Waumini wa dini ya Kiislamuwakiwa kwenye sala ya Eid el-fitr huko Geita

Reactions:

0 comments:

Post a Comment