Friday, 1 May 2015


DSC_0107
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiendesha mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Na Mwandishi Wetu, Sengerema
AWAMU ya pili ya mradi wa kuwezesha redio za jamii kuhamasisha wananchi kushiriki katika kilimo, afya na elimu unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu baada ya awamu ya kwanza ya miaka mitatu kuonesha mafanikio makubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, wakati akihojiwa kuhusiana na mafunzo ya Tehama kwa Mawakala wa habari wa Redio za Jamii nchini yanayofanyika mjini hapa.
Alisema japo mradi huo umemalizika, kumekuwepo na mabadiliko mengi katika uendeshaji wa redio hizo za jamii ikiwa ni pamoja na matumizi ya Tehama katika kutengeneza vipindi na kuvirusha.
Mradi huo wa uwezeshaji wa miaka mitatu ulimalizwa kwa mafunzo ya siku nne katika kituo cha redio jamii cha Sengerema Telecentre ambapo washiriki kutoka redio 9 walijifunza matumizi ya teknolojia katika kutengeneza vipindi, kukusanya taarifa kwa kutumia simu za kawaida na namna ya kuendesha redio hizo kuwa na mvuto na kutengeneza mpango kazi wa biashara.
Mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na Unesco na shirika la maendeleo la Sweden ( SIDA) limelenga kumwezesha mfanyakazi wa redio kutumia simu za mkononi kukusanya na kuboresha habari zake na kuzituma katika redio kwa matumizi ya ushawishi.
“Tumeona mafanikio makubwa kwani kwa sasa wawakilishi wa redio hizi wanaweza kutengeneza vipindi kwa kuwashirikisha wanavijiji kutoa sauti zao ili zisikike,” alisema kutokana na hilo redio hizo sasa zimekuwa maarufu na za kuaminika.
Alisema nia ya Unesco ni kuhakikisha kwamba redio hizo zinashiriki kikamilifu katika kuhakikisha wananchi wanatoa na kupata taarifa zinazoweza kutumiwa na redio hizo kuhamasisha shughuli mbalimbali zikiwemo za kiafya, kielimu na kilimo.
DSC_0025
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akitoa maelekezo kwa vikundi kazi wakati mafunzo hayo.
Miongoni mwa washiriki wa semina ya mwisho Pili Mlindwa wa redio jamii ya Panga FM akizungumzia mafunzo waliyopewa katika matumizi ya Tehama, alisema yamembadili sana katika utendaji wake na kumuongezea maarifa ya kazi.
Alisema amefurahishwa sana na mafunzo ya Tehama ambayo sasa anaweza akafanya kazi nje ya studio na bado mhariri wake akawa na taarifa yake na kuitumia.
Alisema mafunzo mengi aliyopata katika mradi huo yakiwemo pia ya matumizi ya meseji Matrix, simu za mkononi kukusanya na kutoa taarifa kumemfanya awe wa kujiamini.
Naye mwandishi wa habari, Bakari Khalid wa redio jamii Kaham FM ya Shinyanga akizungumzia Mafunzo ya Tehama alisema kwamba Unesco imefanya jambo la maana kuwapa mafunzo hayo ikizingatiwa kwamba redio nyingi zina watu wasiopitia chuo.
Alisema kwa sasa wanaweza kutengeneza vipindi bora vya kuhamasisha afya, elimu na kilimo na namna ya kuandika habari.
Aidha alisema sasa wana uwezo wa kutumia kompyuta mpanguso (tablet) katika kuandaa vipindi na pia kuandaa taarifa mbalimbali.
DSC_0142
Wakala wa habari wa kituo cha Orkonerei Radio Service (ORS) cha wilayani Simanjiro, Nyangusi Ole Sangida akichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili Mawakala wa Redio Jamii katika ukusanyaji wa habari wakati wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0019
Wakala wa habari wa kituo cha redio jamii Pangani FM, Pili Mlindwa akichangia mada wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku nne ikiwa ni sehemu ya mradi wa SIDA wa kuwajengea uwezo katika kuwawezesha kutengeneza vipindi bora.
DSC_0270
Wakala wa habari wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Paulina Juma akiwasilisha kazi ya kikundi ya kuandaa habari na kurekodi kipindi waliyofanya kwa vitendo katika Kompyuta mpanguso (Tablet) walizokuwa wakitumia kwenye mafunzo hayo.
DSC_0096
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
DSC_0122
Baadhi ya mawakala wa habari wa vituo vya redio jamii wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Kompyuta mpanguso (Tablet) wakati wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0252
Baadhi ya mawakala wa habari kutoka vituo mbalimbali va redio jamii nchini wakiwa katika za vikundi.
DSC_0057
Wakala wa habari wa kituo cha Redio Jamii Pambazuko FM, Kaima Akida akifanya "Recap" ya mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (hayupo pichani).
DSC_0292
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza machache wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa mawala wa redio jamii nchini ambapo aliwaasa kuyazingatia na kuyafanyia kazi waliyojifunza pindi warudipo kwenye vituo vyao vya kazi. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
DSC_0314
Wakufunzi na washiriki wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment