Friday, 1 May 2015

Wafanyakazi wakishikana mikono kuonyesha mshikamano wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani almaarufu kama "May Day" kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, leo Ijumaa Mei 1, 2015. Sherehe hizo zilifanyika kitaifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambako Rais Jakaya Kikwete, alikuwa mgeni rasmi. Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Rais amewataka wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga kura na akawataka wananchi kjuipigia kura ya ndio katiba pendekezwa

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) pamopja na Viongozi wengine wakinyanyua mikono  juu wakati wakiimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba.

Maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi Kisiwani Pemba yakiingia katika uwanja wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chakechake leo wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi kisiwani Pemba wakati akilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba
Mashamsham ya siku ya wafanyakazi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ni mbio za kuku hizo, ;picha ya chini pia


Maandamano ya wafanyakazi yakiingia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Doaoma

Mfano wa kikao cha bunge, wafanyakazi wa bunge wakionyesha shughuliza vikao hivyo zinavyoendeshwa

Wajasiriamali wachanganya zege

Maandamano ya wafanyakazi wa mkoa wa Dodoma yakiingia uwanja wa Jamhuri

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akihutubia wananhi uwanja wa Uhuru jijini

Brass band ya JKT Makutupora, ikiongoza maandamano kjuingia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Mpambe wa bunge akionyesha umahiri wake

Wafanyakazi

Mbio za kuku
Rais Jakaya Kikwete, akihutubia maelfu ya wafanyakazi na wakazi wa jiji la Mwanza kwenye kilelel cha sikukuu ya Wafanyakazi kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini humo Ijumaa Mei 1, 2015

Walimu wakifikisha ujumbe kwa Rais, kwenye uwanja wa CCM-Kirumba

Machinga nao walikuwepo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu toka kwa Gratian Mukoba, Rais wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wakati wa kilele cha Mei Mosi Uwanja wa CCM Kirumbna jijini Mwanza leo mei 1, 2015.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment