Monday, 24 November 2014

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea baada ya kupokea salamu maalum kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama, zikimtakiamtakia kheri, baada ya kufanyiwa upasuajiwa tezi dume kwenye hospitali ya Johns Hopckins huko Baltimore, Marylandna. Ujumbe wa Rais Obama, uliwasilishwa kwa Rais Kikwetena balozi wa Tanzania nchini Marekani,  Liberata

Rais Kikwete akimkaribisha balozi Mulamula na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, wakati balozi huyo alipompelekea salamu za kheri Rais Kikwete, zilizotoka kwa Rais wa Marekani Obama

Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  baadhi ya wafanyakazi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati
walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata
Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri
na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore,
Maryland, Marekani.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha
kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya
njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo  jijini Baltimore,
Maryland, Marekani.


Rais akiwa mwenye furaha tele

Rais akipokea salamu hizo

Rais akisoma salamu za rais mwenzake Barack Obama

Reactions:

0 comments:

Post a Comment