Monday, 24 November 2014

Baba mwenye mtoto, Erick Kamanzi, (Kushoto), akiwa na watoto wake, Kulia ni mtoto wa miaka 2 aliyepigwa na kuteswa na msichana wa kazi huko Uganda


MWNAMKE mfanyakazi wa ndani Jolly Tumuhiirwe, ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alivuma kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kitendo chake cha kinyama cha kumpiga mtoto wa “Mdosi” wake jijini Kampala Uganda, amekamatwa na polisi tayari imemfungulia mashtaka ya utesaji.
Hata hivyo polisi wanatoa pendekezo jipya kwa mwendesha mashtaka nchini Uganda, ili mashtaka hayo yabadilishwe na kuwa ya kujaribu kuua.
Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 22, alifanya kituko kisichotarajiwa na wengi walioiona video iliyomnasa kutoka kamera ya siri iliyotegeshwa na bosi wake bila yeye kujua.
Msichana huyo mzaliwa wa wilaya ya Rukungiri alikuwa ameajiriwa na Erick Kamanzi ambaye anafanya kazi kwenye shirika moja lisilo la kiserikali jijini Kampala.

Video hiyo ilionyesha, msichana huyo wa “kazi”, akimlisha kwa shuruti mototo huyo wa kike mwenye umri wa miaka 2, na kutokana na kasi ya ulishaji, mtoto huyo alishindwa kuhimili vijiko na hapo akaanza kutapika.

Kitendo cha mtoto huyo kutapika, kilichokoza mikono ya msichana huyo, aliyeanza kumzaba vibao vya usoni kabla ya kumrusha sakafuni na kuanza kumtandika kwenye makalio na kitu ambacho hakijulikani kabla ya kuanza kumpiga mateke na kumkanyaga mgongoni.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment