Tuesday, 11 March 2014

Rais Jakaya Kikwete, akitoa hotuba katika hafla ya kupokea msada wa magari 11 aina ya Land Rover Ikulu jijini Dar es Salaam, Jumanne Machi 11, 2014. Jumuiya ya Uhifadhi Wanyama ya Frankfurt Zoological Society (FZS) ya nchini Ujerumani, ndiyo iliyotoa msaada huo ambapo katika hotuba yake ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa FZS, Robert Muir, alisema, wakati idadi ya Tembo na Faru inazidi kuporomoka, FZS itaendelea kuongeza misaada yake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya ujangili. Alisema, msaada huo wa magari utasaidia shughuli za doria kwenye pori la hifadhi la Selou, Maswa na mbuga ya wanayama ya Serengeti. Katika hafla hiyo, iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Balozi wa Jumuiya ya Ulaya, Filiberto Sebregondi, Balozi mdogo wa Ujerumani nchini, Hans Koeppel, na maafisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wale wa Ujerumani, ilifanyika kwenye viwanja vya Ikulu.

Mkurugenzi wa FZS, Robert Muir akitoa hotuba yake

Balozi mdogo wa Ujerumani nchini, Hans Koeppel, akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya, Filiberto Sebregondi

Magari hayo yakiwa yamepangwa kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Kikwete

Rais Kikwete, akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa FZS robert Muir kwa mazungumzo kabla ya kupokea msada wa magari hayo

Rais Kikwete, akiwa kwenye mazungumzo yake na mgeni wake Muir

Rais Kikwete akiyatazama magari hayo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment